Quran with Swahili translation - Surah Fussilat ayat 44 - فُصِّلَت - Page - Juz 24
﴿وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا أَعۡجَمِيّٗا لَّقَالُواْ لَوۡلَا فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥٓۖ ءَا۬عۡجَمِيّٞ وَعَرَبِيّٞۗ قُلۡ هُوَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ هُدٗى وَشِفَآءٞۚ وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٞ وَهُوَ عَلَيۡهِمۡ عَمًىۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُنَادَوۡنَ مِن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ ﴾
[فُصِّلَت: 44]
﴿ولو جعلناه قرآنا أعجميا لقالوا لولا فصلت آياته أأعجمي وعربي قل هو﴾ [فُصِّلَت: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau tungaliifanya hii Qur’ani tuliyokuteremshia, ewe Mtume, ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu, washirikina wangalisema, «Je, si zifafanuliwe aya zake tupate kuzifahamu na kuzijua? Ni vipi hii Qur’ani ni kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu na hali lugha ya huyu aliyeteremshiwa ni ya Kiarabu? Hili haliwi!» Waambie, ewe Mtume, «Hii Qur’ani, kwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ni uongofu kutoka kwenye upotevu na ni ponyesho la yaliyomo vifuani ya shaka na magonjwa. Na wale wasioiamini Qur’ani kuna uziwi ndani ya mashikio yao unaowafanya wasiisikie na wasiizingatie; nayo (hiyo Qur’ani) ni upofu kwao wa nyoyo zao, hawaongoki kwayo.» Basi washirikina hao ni kama yule anayeitwa naye yuko mahali mbali, hamsikii mwenye kulingania wala hamuitiki mwenye kuita |