Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 27 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿لَّقَدۡ صَدَقَ ٱللَّهُ رَسُولَهُ ٱلرُّءۡيَا بِٱلۡحَقِّۖ لَتَدۡخُلُنَّ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمۡ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَۖ فَعَلِمَ مَا لَمۡ تَعۡلَمُواْ فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتۡحٗا قَرِيبًا ﴾
[الفَتح: 27]
﴿لقد صدق الله رسوله الرؤيا بالحق لتدخلن المسجد الحرام إن شاء الله﴾ [الفَتح: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika Mwenyezi Mungu Alimsadikishia Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ndoto yake aliyomuotesha kwa haki kwamba utaingia, wewe na Maswahaba wako, Nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa mko katika amani, hamuwaogopi watu wa ushirikina, hali ya kuwa mnanyoa vichwa vyenu na mnapunguza. Mwenyezi Mungu Alijua kheri na maslahi ya kuwaepusha nyinyi na Makkah mwaka wenu huo na kuingia huko baadae, msiyoyajua nyinyi, na Akajaalia, kabla ya kuingia kwenu Makkah mliyoahidiwa, ufunguzi wa karibu, nao ni mapatano ya amani ya Ḥudaybiyah na ufunguzi wa Khaybar |