Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 26 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿إِذۡ جَعَلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَأَلۡزَمَهُمۡ كَلِمَةَ ٱلتَّقۡوَىٰ وَكَانُوٓاْ أَحَقَّ بِهَا وَأَهۡلَهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا ﴾
[الفَتح: 26]
﴿إذ جعل الذين كفروا في قلوبهم الحمية حمية الجاهلية فأنـزل الله سكينته﴾ [الفَتح: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Pindi wale waliokanusha walipoingiza ndani ya nyoyo zao ghera, ghera za watu wa zama za ujinga, ili wasikubali utume wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na miongoni mwa hayo ni kule kukataa kwao kwandika «Bi ism Allāh al-Raḥmān al-Raḥīm» katika mapatano ya Ḥudaybiyah, na wakakataa kuandika, «Haya ndiyo yale aliyoyapitisha Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu.» Na Mwenyezi Mungu Akamteremshia utulivu Mtume Wake na Waumini pamoja na yeye, Akawathibitishia neno «Lā ilāha illā Allāh» ambalo ndio kichwa cha ya kila uchamungu. Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Waumini pamoja na yeye ndio wanaostahiki zaidi neno la uchamungu kuliko washirikina. Na hivyo ndivyo walivyokuwa, walistahiki neno hili na sio washirikina. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa ujuzi wa kila kitu, hakuna kitu chochote kinachofichamana Kwake |