Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 19 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ عَلَىٰ فَتۡرَةٖ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُواْ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٖ وَلَا نَذِيرٖۖ فَقَدۡ جَآءَكُم بَشِيرٞ وَنَذِيرٞۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ﴾
[المَائدة: 19]
﴿ياأهل الكتاب قد جاءكم رسولنا يبين لكم على فترة من الرسل أن﴾ [المَائدة: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi Mayahudi na Wanaswara, amewajia mjumbe wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, ili kuwafunulia haki na uongofu baada ya kipindi kirefu cha wakati baina ya kumtuma yeye na kumtuma ‘Īsā mwana wa Maryam, ili msije mkasema, «Hakutujia mjumbe, mwenye kutoa bishara wala mwenye kuonya.» Hakika ashawajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mjumbe anayempa bishara njema mwenye kumuamini na anayemuonya mwenye kumuasi. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, wa kumtesa mwenye kuasi na kumpa thawabu mwenye kutii |