Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 20 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَعَلَ فِيكُمۡ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكٗا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمۡ يُؤۡتِ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[المَائدة: 20]
﴿وإذ قال موسى لقومه ياقوم اذكروا نعمة الله عليكم إذ جعل فيكم﴾ [المَائدة: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, pindi aliposema Mūsā, amani imshukie, kuwaambia watu wake, «Enyi Wana wa Isrāīl, Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu, pindi Alipochagua Manabii kati yenu, Akawafanya wafalme, mnayatawala mambo yenu baada ya kuwa mumetawaliwa na Fir‘aun na watu wake. Na hakika Aliwatunuku nyinyi aina mbalimbali za neema ambazo Hakumtunuku nazo yoyote miongoni mwa walimwengu wa zama zenu |