×

Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa 5:3 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:3) ayat 3 in Swahili

5:3 Surah Al-Ma’idah ayat 3 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 3 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَٰمِۚ ذَٰلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَئِسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗاۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِي مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٖ لِّإِثۡمٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[المَائدة: 3]

Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: حرمت عليكم الميتة والدم ولحم الخنـزير وما أهل لغير الله به والمنخنقة, باللغة السواحيلية

﴿حرمت عليكم الميتة والدم ولحم الخنـزير وما أهل لغير الله به والمنخنقة﴾ [المَائدة: 3]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Amewaharamishia mfu, naye ni mnyama aliyekufa mwenyewe bila ya kuchinjwa. Na pia Amewaharamishia nyinyi damu inayotiririka inayomwagwa, nyama ya nguruwe, mnyama ambaye wakati wa kuchinjwa ametajiwa jina lisilokuwa la Mwenyezi Mungu, mnyama aliyenyongwa kwa kuzibwa pumzi zake mpaka akafa, mnyama aliyekufa kwa kupigwa gongo au jiwe, mnyama aliyeanguka kutoka mahali pa juu au aliyeanguka kisimani akafa na mnyama aliyekufa kwa kupigwa pembe na mwenzake. Na pia Amewaharamishia mnyama aliyeliwa na mnyama mwingine kama simba, chuimarara, mbwamwitu na mfano wake. Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, Amewatoa, miongoni mwa wale Aliowaharamisha, kuanzia wale walionyongeka na waliofuatia, wale mliowahi kuwachinja kabla hawajafa, hao ni halali kwenu. Na Amewaharamishia nyinyi wanyama waliochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa vitu vilivyosimamishwa viabudiwe, viwe ni mawe au vinginevyo. Na Amewaharamishia kutaka kujua mambo, mliyoandikiwa na msiyoandikiwa, kwa viapo; navyo ni vipande ambavyo walikuwa wakitaka uamuzi kwavyo wakitaka kufanya jambo kabla hawajalifanya. Hayo mliyotajiwa katika aya hii kati ya yaliyoharamishwa, yakifanywa, huwa ni kutoka kwenye amri ya Mwenyezi Mungu na twaa Yake na kwenda kwenye maasia. Sasa imekatika tamaa ya makafiri kwamba nyinyi mtaiacha Dini yenu muende kwenye ushirikina baada ya mimi kuwapa ushindi juu yao. Basi msiwaogope wao na mniogope mimi. Leo nimeshawakamilishia dini yenu, Dini ya Uislamu, kwa kuuhakikisha ushindi na kuikamilisha Sheria, nimewatimizia neema zangu kwenu kwa kuwatoa kwenye giza la ujinga na kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani na nimewaridhia kwamba Uislamu ndio Dini, basi shikamaneni nayo wala msiiache. Na yule aliyepatikana na dharura ya njaa ikambidi ale mfu, na akawa hakukusudia kutenda kosa, basi inafaa kwake kumla. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek