×

Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu 5:2 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:2) ayat 2 in Swahili

5:2 Surah Al-Ma’idah ayat 2 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 2 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحِلُّواْ شَعَٰٓئِرَ ٱللَّهِ وَلَا ٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَلَا ٱلۡهَدۡيَ وَلَا ٱلۡقَلَٰٓئِدَ وَلَآ ءَآمِّينَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّهِمۡ وَرِضۡوَٰنٗاۚ وَإِذَا حَلَلۡتُمۡ فَٱصۡطَادُواْۚ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ أَن صَدُّوكُمۡ عَنِ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ أَن تَعۡتَدُواْۘ وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[المَائدة: 2]

Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha toka Hija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا لا تحلوا شعائر الله ولا الشهر الحرام ولا الهدي, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا لا تحلوا شعائر الله ولا الشهر الحرام ولا الهدي﴾ [المَائدة: 2]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuta sheria Zake kivitendo, msivuke mipaka ya Mwenyezi Mungu na alama Alizoziwekea hiyo mipaka yake. Na msihalalishe vita katika miezi mitukufu, nayo ni Mfungopili, Mfungotatu, Mfungone na Rajabu- na hilo lilikuwa katika mwanzo wa Uislamu-. Na msivunje heshima ya wanyama waliokusudiwa kuchinjwa katika ibada ya Hija, wala msivunje heshima ya vitu walivyovishwa navyo. Kwani walikuwa wakiwavalisha kwenye shingo zao miseja ya sufi au ya nyoya, ikiwa ni kitambulisho kwamba mnyama huyo ni wa kuchinjwa katika ibada ya Hija na kwamba mwenye mnyama anaenda Hija. Wala msihalalishe kuwapiga vita wenye kuikusudia Nyumba tukufu, ambao wanazitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu zinazowatengezea maisha yao na kumridhisha Mola wao. Na pindi mnapomaliza ibada yenu ya Hija, mnahalalishiwa kuwinda. Na isiwapelekee nyinyi kuwachukia baadhi ya watu kwa kuwa waliwazuia nyinyi kufika Msikiti mtukufu, kama ilivyotokea katika mwaka wa Hudaibiyah, kuacha kuwafanyia uadilifu. Na saidianeni kati yenu, enyi Waumini, kufanya wema na kumcha Mwenyezi Mungu wala msisaidiane kwenye mambo ya madhambi, maasia na kuivuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na jihadharini kuenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ni Mkali wa kutesa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek