Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 5 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿ٱلۡيَوۡمَ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُۖ وَطَعَامُ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ حِلّٞ لَّكُمۡ وَطَعَامُكُمۡ حِلّٞ لَّهُمۡۖ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِيٓ أَخۡدَانٖۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ حَبِطَ عَمَلُهُۥ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ ﴾
[المَائدة: 5]
﴿اليوم أحل لكم الطيبات وطعام الذين أوتوا الكتاب حل لكم وطعامكم حل﴾ [المَائدة: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu kwenu leo hii, enyi Waumini, ni kwamba Amewahalalishia vilivyo halali vizuri. Na vichinjwa vya Mayahudi na Wanaswara, iwapo watawachinja wanyama wao kuambatana na sheria yao, ni halali kwenu ; na vichinjwa vyenu ni halali kwao. Na Amewahalalishia nyinyi, enyi Waumini, kuwaoa wanawake wanaojihifadhi, nao ni wale walio huru kati ya wanawake Waumini wanaojizuia na uzinifu. Vilevile ni halali kuwaoa wanawake walio huru wanaojiepusha na uzinifu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, iwapo mtawapa mahari yao na mkawa mumejihifadhi kwa kutofanya uzinifu na kuweka mahawara na mkawa mumejiaminisha kuwa hamutaathirika na dini yao. Na mwenye kuzikataa sheria za fmani, basi vitendo vyake vimishaharibika, na yeye, Siku ya Kiyama, atakuwa ni miongoni mwa wenye kupata hasara |