×

Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo 5:64 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:64) ayat 64 in Swahili

5:64 Surah Al-Ma’idah ayat 64 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 64 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ يَدُ ٱللَّهِ مَغۡلُولَةٌۚ غُلَّتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْۘ بَلۡ يَدَاهُ مَبۡسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيۡفَ يَشَآءُۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ طُغۡيَٰنٗا وَكُفۡرٗاۚ وَأَلۡقَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ كُلَّمَآ أَوۡقَدُواْ نَارٗا لِّلۡحَرۡبِ أَطۡفَأَهَا ٱللَّهُۚ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادٗاۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ﴾
[المَائدة: 64]

Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo fumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya waliyo yasema. Bali mikono yake iwazi. Hutoa apendavyo. Kwa yakini yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru. Na Sisi tumewatilia uadui na chuki baina yao mpaka Siku ya Kiyama. Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi waharibifu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وقالت اليهود يد الله مغلولة غلت أيديهم ولعنوا بما قالوا بل يداه, باللغة السواحيلية

﴿وقالت اليهود يد الله مغلولة غلت أيديهم ولعنوا بما قالوا بل يداه﴾ [المَائدة: 64]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Anamjulisha Mtume Wake sehemu ya makosa ya Mayahudi, kitu walichokuwa wakikizungumza kwa siri baina yao, kuwa wao walisema, «Mkono wa Mwenyezi Mungu umefungwa kutotenda mema, Ametufanyia ubahili riziki kwa kutubania na kutotupanulia.» Walisema hilo wakati walipopatwa na ukame na ukosefu wa mvua. Mikono yao ndiyo iliyofungwa, kwa maana: mikono yao imezuiliwa kutenda mema, na Mwenyezi Mungu Amewafukuza kutoka kwenye rehema Yake kwa sababu ya neno lao. Mambo sivyo kama wanavyomzulia Mola wao, bali mikono Yake miwili imekunjuliwa, haikuzuiliwa wala hakuna pingamizi ya kumzuia kutoa. Kwani Yeye ni Mpaji, ni Karimu, Anatoa kulingana na hekima na yale yenye maslahi kwa waja. Kwenye aya hii kuna thibitisho la sifa ya Mikono miwili kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasita na kila sifa ya upungufu na kutukuka, kama inavyolingana na Yeye, pasi na kufananisha wala kueleza namna ilivyo. Lakini wao watazidi ukiukaji mipaka na ukafiri kwa sababu ya chuki yao na uhasidi wao kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amekuchagua wewe kwa utume. Mwenyezi Mungu Anayatolea habari makundi ya Mayahudi kwamba wao wataendelea, mpaka Siku ya Kiyama, kufanyiana uadui wao kwa wao na kuchukiana wao kwa wao. Kila wanapopanga njama ya kuwafanyia vitimbi Waislamu, kwa kuzusha fitina na kuuwasha moto wa vita, Mwenyezi Mungu Anavikomesha vitimbi vyao na kuutenganisha mkusanyiko wao. Na Mayahudi hawataacha kuendelea kumuasi Mwenyezi Mungu kwa kufanya yanayoleta uharibifu na misukosuko katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hawapendi waharibifu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek