Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 12 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نَٰجَيۡتُمُ ٱلرَّسُولَ فَقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَةٗۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ فَإِن لَّمۡ تَجِدُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴾
[المُجَادلة: 12]
﴿ياأيها الذين آمنوا إذا ناجيتم الرسول فقدموا بين يدي نجواكم صدقة ذلك﴾ [المُجَادلة: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Mkitaka kusema na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa siri baina yenu na yeye, basi tangulizeni kabla ya hilo kutoa sadaka kwa wahitaji. Hilo ni bora kwenu, kwa kuwa lina thawabu, na lenye kusafisha zaidi nyoyo zenu na madhambi. Basi mkitopata cha kutoa sadaka hamna makosa juu yenu. Kwani Mwenyezi Mungu, kwa hakika, ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake Waumini, ni Mwenye huruma kwao |