Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 13 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿ءَأَشۡفَقۡتُمۡ أَن تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَٰتٖۚ فَإِذۡ لَمۡ تَفۡعَلُواْ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ﴾
[المُجَادلة: 13]
﴿أأشفقتم أن تقدموا بين يدي نجواكم صدقات فإذ لم تفعلوا وتاب الله﴾ [المُجَادلة: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, mmeogopa kuwa mtafukarika mkitanguliza sadaka kabla ya kunong’ona na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi msipofanya hilo mliloamrishwa, na Mwenyezi Mungu Amewasamehe na Amewaruhusu msilifanye hilo, basi simameni imara na muendelee kusimamisha Swala, kutoa Zaka na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kila lile mliloamrishwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa Matendo yenu na ni Mwenye kuwalipa kwayo |