Quran with Swahili translation - Surah Al-Mujadilah ayat 4 - المُجَادلة - Page - Juz 28
﴿فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينٗاۚ ذَٰلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴾
[المُجَادلة: 4]
﴿فمن لم يجد فصيام شهرين متتابعين من قبل أن يتماسا فمن لم﴾ [المُجَادلة: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Asiyepata shingo ya kuiacha huru, basi lililo wajibu kwake ni kufunga miezi miwili iliyofuatana kabla hajamuundama mkewe. Na asiyeweza kufunga miezi miwili kwa udhuru wa kisheria, basi na awalishe masikini sitini chakula kinachowashibisha. Hayo tuliyoyaelezea nyinyi ya hukumu ya kujiharamishia mke wake kwa kumfananisha na mgongo wa mamake ni kwa sababu mmuamini Mwenyezi Mungu na mumfuate Mtume Wake na mfanye matendo yanayoambatana na Sheria ya Mwenyezi Mungu na muache yale ambayo mlikuwa mkiyafanya wakati mlipokuwa kwenye ujinga. Hukumu hizo zilizotajwa ndizo amri za Mwenyezi Mungu na mipaka Yake, basi msiikiuke. Na wenye kuzikataa watapata adhabu yenye uchungu |