Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 10 - الحَشر - Page - Juz 28
﴿وَٱلَّذِينَ جَآءُو مِنۢ بَعۡدِهِمۡ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا وَلِإِخۡوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَا تَجۡعَلۡ فِي قُلُوبِنَا غِلّٗا لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٞ رَّحِيمٌ ﴾
[الحَشر: 10]
﴿والذين جاءوا من بعدهم يقولون ربنا اغفر لنا ولإخواننا الذين سبقونا بالإيمان﴾ [الحَشر: 10]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na waliokuja miongoni mwa Waumini baada ya Anṣār na Muhājirūn wanasema, «Mola wetu! Tusamehe dhambi zetu, na uwasamehe ndugu zetu katika Dini waliotutangulia katika kuamini, Na usitie ndani ya nyoyo zetu uhasidi na chuki kwa yoyote miongoni mwa wenye kuamini. Mola wetu! Wewe ni Mpole kwa waja wako. Unawarehemu waja wako rehema rehema kunjufu katika maisha yao ya hapa ulimwenguni ya kesho Akhera.» Katika hii aya pana dalili kwamba inapasa kwa Muislamu awataje kwa wema wale waliomtangulia na awaombee dua, na awapende maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na awataje kwa wema na awaombee radhi ya Mwenyezi Mungu |