Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 11 - الحَشر - Page - Juz 28
﴿۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نَافَقُواْ يَقُولُونَ لِإِخۡوَٰنِهِمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَئِنۡ أُخۡرِجۡتُمۡ لَنَخۡرُجَنَّ مَعَكُمۡ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمۡ أَحَدًا أَبَدٗا وَإِن قُوتِلۡتُمۡ لَنَنصُرَنَّكُمۡ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ﴾
[الحَشر: 11]
﴿ألم تر إلى الذين نافقوا يقولون لإخوانهم الذين كفروا من أهل الكتاب﴾ [الحَشر: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je huwatazami hao wanafiki wanawaambia ndugu zao katika ukafiri miongoni mwa Mayahudi wa Banū al Naḍī, «Tunaapa kwamba Muhammad na walio pamoja na yeye wakiwatoa kutoka majumbani mwenu tutatoka na nyinyi! Na hatutamfuata yoyote kuhusu nyinyi anayetutaka tusiwasaidie au tuache kutoka pamoja na nyinyi, na wakipigana na nyinyi tutawasaidia juu yao?» na Mwenyezi Mungu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika yale waliyowaahidi Banū al Naḍī |