×

Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji 6:145 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:145) ayat 145 in Swahili

6:145 Surah Al-An‘am ayat 145 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 145 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿قُل لَّآ أَجِدُ فِي مَآ أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٖ يَطۡعَمُهُۥٓ إِلَّآ أَن يَكُونَ مَيۡتَةً أَوۡ دَمٗا مَّسۡفُوحًا أَوۡ لَحۡمَ خِنزِيرٖ فَإِنَّهُۥ رِجۡسٌ أَوۡ فِسۡقًا أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[الأنعَام: 145]

Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل لا أجد في ما أوحي إلي محرما على طاعم يطعمه إلا, باللغة السواحيلية

﴿قل لا أجد في ما أوحي إلي محرما على طاعم يطعمه إلا﴾ [الأنعَام: 145]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Sema, ewe Mtume, mimi sipati, kati ya yale aliyoniletea wahyi Mwenyezi Mungu, kitu kilicho haramu kwa mwenye kukila, kati ya vile mnavyovitaja kwamba vimeharamishwa miongoni mwa wanyama howa, isipokuwa awe amekufa bila kuchinjwa, au ni damu itiririkayo, au iwe ni nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni najisi, au akawa ni mnyama ambaye kuchinjwa kwake kumetoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama akiwa mnyama aliyechinjwa ametajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kuchinjwa. Basi mwenye kulazimika kula chochote kati ya hizo zilizoharamishwa kwa dharura ya njaa kali, pasi na kutaka kujifurahisha wala kukiuka mpaka wa dharura, hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni mwenye kumsamehe, ni mwenye huruma naye. Na hakika imethibiti, baadaye, kwa mafundisho ya Mtume kuwa ni haramu kula kila mnyama mwitu anayewinda kwa kutumia meno, kila ndege anayewinda kwa kutumia kucha, punda na mbwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek