Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 146 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٖۖ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ وَٱلۡغَنَمِ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتۡ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلۡحَوَايَآ أَوۡ مَا ٱخۡتَلَطَ بِعَظۡمٖۚ ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِبَغۡيِهِمۡۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ ﴾
[الأنعَام: 146]
﴿وعلى الذين هادوا حرمنا كل ذي ظفر ومن البقر والغنم حرمنا عليهم﴾ [الأنعَام: 146]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na watajie washirikina hawa, ewe Mtume, wanyama na ndege tuliowaharamishia Mayahudi: nao ni kila ambaye hana pasuko vidoleni mwake, kama ngamia na mbuni, na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo isipokuwa yale mafuta yaliyoshikana na migongo ya wanyama hao na tumbo zao, au yaliyoshikana na mfupa wa mkia na mbavu na mfano wake. Uharamishaji huu uliotajwa juu ya Mayahudi ni adhabu kutoka kwetu kwa sababu ya matendo yao maovu. Na sisi ni wakweli kwa yale tuliyoyaeleza kuhusu wao |