Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 155 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ ﴾
[الأنعَام: 155]
﴿وهذا كتاب أنـزلناه مبارك فاتبعوه واتقوا لعلكم ترحمون﴾ [الأنعَام: 155]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hii Qur’ani ni kitabu tulichokiteremsha kwa Nabii wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kheri yeke ni nyingi. Basi kifuateni kwa yale anayowaamrisha na kuwakataza. Na muogopeni Mwenyezi Mungu msije mkaenda kinyume na amri Yake yoyote, kwa matumaini kuwa mtarehemewa na mtaokolewa na adhabu Yake na mpate malipo Yake mema |