Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 30 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ قَالَ أَلَيۡسَ هَٰذَا بِٱلۡحَقِّۚ قَالُواْ بَلَىٰ وَرَبِّنَاۚ قَالَ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ ﴾
[الأنعَام: 30]
﴿ولو ترى إذ وقفوا على ربهم قال أليس هذا بالحق قالوا بلى﴾ [الأنعَام: 30]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau utawaona, ewe Mtume, wenye kukanusha kufufuliwa watakapofungwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ili uamuzi wa Mwenyezi Mungu upite kuhusu wao Siku ya Kiyama, ungaliona hali mbaya sana, pindi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atakaposema, «Je, ufufuzi huu, mliokuwa mkiukanusha ulimwenguni, si kweli?» Watasema, «Kwani? Tunaapa kwa Mola wetu kuwa huu ni kweli.» Hapo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema, «Basi onjeni adhabu kwa mlivyokuwa mkikufuru,» yaani, adhabu ambayo mlikuwa mkiikanusha ulimwenguni kwa sababu ya kumkataa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |