Quran with Swahili translation - Surah At-Taghabun ayat 12 - التغَابُن - Page - Juz 28
﴿وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ﴾
[التغَابُن: 12]
﴿وأطيعوا الله وأطيعوا الرسول فإن توليتم فإنما على رسولنا البلاغ المبين﴾ [التغَابُن: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mtiini Mwenyezi Mungu, enyi watu, na muongokee Kwake katika yale Aliyoyaamrisha na Aliyoyakataza, na mfuateni Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, katika yale aliyowafikishia kutoka kwa Mola wake. Na iwapo mtaupa mgongo utiifu wenu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, basi Mjumbe wetu hana madhara yoyote kutokana na kupa mgongo kwenu. Jukumu lake yeye ni kuwafikishia nyinyi yale Aliyotumilizwa kwayo ufikishaji wenye maelezo ya waziwazi |