Quran with Swahili translation - Surah AT-Talaq ayat 12 - الطَّلَاق - Page - Juz 28
﴿ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّۖ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَهُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عِلۡمَۢا ﴾
[الطَّلَاق: 12]
﴿الله الذي خلق سبع سموات ومن الأرض مثلهن يتنـزل الأمر بينهن لتعلموا﴾ [الطَّلَاق: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Aliyeziumba mbingu saba na Akaumba ardhi saba, na Akateremsha amri kupitia wahyi Aliyowateremshia Mitume Wake na kwa yale Anayowapangia viumbe Vyake kwayo kati ya mbingu na ardhi, ili mpate kujua , enyi watu, kwamba Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda na kwamba Mwenyezi Mungu Amekizunguka kila kitu kiujuzi, basi hakuna kitu chochote kilichoko nje ya ujuzi Wake na uweza Wake |