Quran with Swahili translation - Surah AT-Talaq ayat 11 - الطَّلَاق - Page - Juz 28
﴿رَّسُولٗا يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ مُبَيِّنَٰتٖ لِّيُخۡرِجَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ قَدۡ أَحۡسَنَ ٱللَّهُ لَهُۥ رِزۡقًا ﴾
[الطَّلَاق: 11]
﴿رسولا يتلو عليكم آيات الله مبينات ليخرج الذين آمنوا وعملوا الصالحات من﴾ [الطَّلَاق: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ukumbusho huu ni Mtume anayewasomea nyinyi aya za Mwenyezi Mungu zinazowafafanulia haki kwa kuitenga na ubatilifu, ili Apate kuwatoa, wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakazifuata Sheria Zake kivitendo na wakamatii, kutoka kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani. Na yoyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na akafanya matendo mema Atamuingiza kwenye mabustani ya Peponi ambayo chini ya miti yake inapita mito ya maji, wasalie humo milele. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Ameifanya riziki ya Muumini mwema iwe nzuri huko Peponi |