×

Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, 7:143 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:143) ayat 143 in Swahili

7:143 Surah Al-A‘raf ayat 143 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 143 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَٰتِنَا وَكَلَّمَهُۥ رَبُّهُۥ قَالَ رَبِّ أَرِنِيٓ أَنظُرۡ إِلَيۡكَۚ قَالَ لَن تَرَىٰنِي وَلَٰكِنِ ٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡجَبَلِ فَإِنِ ٱسۡتَقَرَّ مَكَانَهُۥ فَسَوۡفَ تَرَىٰنِيۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُۥ لِلۡجَبَلِ جَعَلَهُۥ دَكّٗا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقٗاۚ فَلَمَّآ أَفَاقَ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ تُبۡتُ إِلَيۡكَ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[الأعرَاف: 143]

Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال, باللغة السواحيلية

﴿ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال﴾ [الأعرَاف: 143]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na alipokuja Mūsā kwa wakati uliowekwa nao ni muda wa masiku arubaini na Akasema na yeye Mola wake kwa kumpa wahyi wake, maamrisho Yake na makatazo Yake, alifanya hamu ya kumuona Mwenyezi Mungu akataka amtazame. Mwenyezi Mungu Akamwambia, «Hutoniona!»Yaani hutaweza kuniona ulimwenguni. «Lakini liangalie jabali, likitulia mahali lilipo nitakapolitokezea, basi utaniona.» Alipojitokeza Mola wake kwa lile jabali alilifanya lipondeke liwe sawa na ardhi. Hapo Mūsā alianguka akiwa amezimia. Alipopata fahamu kutoka kwenye hali ya kuzimia alisema, «Kwa kukutakasisha, ewe Mola wangu, na kila sifa isiyolingana na utukufu wako, mimi natubia kwako kutokana na kuomba kwangu kukuona katika uhai huu wa kilimwengu, na mimi ni wa mwanzo wa wenye kukuamini miongoni mwa watu wangu.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek