×

Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo 7:164 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:164) ayat 164 in Swahili

7:164 Surah Al-A‘raf ayat 164 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 164 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ ﴾
[الأعرَاف: 164]

Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإذ قالت أمة منهم لم تعظون قوما الله مهلكهم أو معذبهم عذابا, باللغة السواحيلية

﴿وإذ قالت أمة منهم لم تعظون قوما الله مهلكهم أو معذبهم عذابا﴾ [الأعرَاف: 164]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi kundi kati yao waliposema kuwaambia kundi lingine lililokuwa likiwapa mawaidhia wale waliopita mipaka siku ya Jumamosi na likiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu siku hiyo, «Kwa nini nyinyi mnawaidhia watu ambao Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangamiza ulimwenguni kwa kumuasi au ni Mwenye kuwaadhibu adhabu kali kesho Akhera?» Wakanena wale waliokuwa wakiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu, «Tunawaidhia na tunawakataza ili tuwe na udhuru kuhusu wao na kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Mwenyezi Mungu juu yetu ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kwa matumaini kwamba watamcha Mwenyezi Mungu, watamuogopa na watatubia kutokana na kumuasi kwao Mola wao na kupita mipaka ya mambo yaliyoharamishiwa kwao.»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek