Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 24 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿قُلۡ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ وَإِخۡوَٰنُكُمۡ وَأَزۡوَٰجُكُمۡ وَعَشِيرَتُكُمۡ وَأَمۡوَٰلٌ ٱقۡتَرَفۡتُمُوهَا وَتِجَٰرَةٞ تَخۡشَوۡنَ كَسَادَهَا وَمَسَٰكِنُ تَرۡضَوۡنَهَآ أَحَبَّ إِلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٖ فِي سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ ﴾
[التوبَة: 24]
﴿قل إن كان آباؤكم وأبناؤكم وإخوانكم وأزواجكم وعشيرتكم وأموال اقترفتموها وتجارة تخشون﴾ [التوبَة: 24]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia Waumini, «Iwapo mtawafanya kina baba, watoto, ndugu , wake na jamaa wa karibu, mali mlizozikusanya, biashara ambazo mnaogopa zisikose soko na majumba yanayopendeza ambayo mumekaa ndani yake, (iwapo mtayafanya hayo) ni bora kuliko kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake, basi yangojeni mateso ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake kwenu. Na Mwenyezi Mungu hawapi taufiki wenye kutoka nje ya utiifu Wake |