Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 23 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَابَآءَكُمۡ وَإِخۡوَٰنَكُمۡ أَوۡلِيَآءَ إِنِ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡكُفۡرَ عَلَى ٱلۡإِيمَٰنِۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[التوبَة: 23]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تتخذوا آباءكم وإخوانكم أولياء إن استحبوا الكفر على﴾ [التوبَة: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiwafanye jamaa zenu, miongoni mwa kina baba, watoto na wengineo, kuwa ni marafiki (mnaowategemea) mkawa mnawasambazia siri za Waislamu na mnawataka ushauri katika mambo yenu, iwapo bado wako kwenye ukafiri na kuufanyia uadui Uislamu. Na yoyote atakayewafanya wao kuwa ni marafiki na akawapa mapenzi, atakuwa amemuasi Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na ameidhulumu nafasi yake dhuluma kubwa |