Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 39 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿إِلَّا تَنفِرُواْ يُعَذِّبۡكُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَيَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيۡـٔٗاۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ ﴾
[التوبَة: 39]
﴿إلا تنفروا يعذبكم عذابا أليما ويستبدل قوما غيركم ولا تضروه شيئا والله﴾ [التوبَة: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Iwapo hamtatoka, enyi Waumini, kwenda kupigana na adui yenu , Mwenyezi Mungu Atawateremshia mateso Yake na atawaleta watu wengine ambao watatoka kwenda vitani waambiwapo watoke, watamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na nyinyi hamtamdhuru Mwenyezi Mungu chochote kwa kuikimbia kwenu jihadi, kwani Yeye ni mwenye kujitosheleza na nyinyi, na nyinyi ndio wahitaji Wake. Na Analolitaka Mwenyezi Mungu litakuwa hapana budi. Na Mwenyezi Mungu, juu ya kila kitu, ni Muweza, miongoni mwa kutetea dini Yake na Mtume Wake pasi na nyinyi |