Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 54 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَمَا مَنَعَهُمۡ أَن تُقۡبَلَ مِنۡهُمۡ نَفَقَٰتُهُمۡ إِلَّآ أَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأۡتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمۡ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمۡ كَٰرِهُونَ ﴾
[التوبَة: 54]
﴿وما منعهم أن تقبل منهم نفقاتهم إلا أنهم كفروا بالله وبرسوله ولا﴾ [التوبَة: 54]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na sababu ya kutokubaliwa wanavyovitoa ni kwamba wao wameficha ukanushaji wao Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, na ukataaji wao ukweli wa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kwamba wao hawaendi kuswali isipokuwa huku wanaona uzito, na kwamba hawatoi mali yao isipokuwa huku wao ni wenye kuchukia hilo. Wao hawana matarajio ya kupata malipo ya faradhi hizi wala hawaogopi mateso kwa kuziacha kwa ukafiri wao walionao |