Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 84 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰٓ أَحَدٖ مِّنۡهُم مَّاتَ أَبَدٗا وَلَا تَقُمۡ عَلَىٰ قَبۡرِهِۦٓۖ إِنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَمَاتُواْ وَهُمۡ فَٰسِقُونَ ﴾
[التوبَة: 84]
﴿ولا تصل على أحد منهم مات أبدا ولا تقم على قبره إنهم﴾ [التوبَة: 84]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na usimswalie kabisa, ewe Mtume, yoyote aliyekufa miongoni mwa wanafiki na usisimame kwenye kaburi yake kumuombea, kwa kuwa wao wamemkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na wamekufa na wao wametoka kwenye utiifu. Hii ni hukumu yenye kuenea kwa kila mtu ambaye unafiki wake umejulikana |