×

Surah Al-Muddaththir in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Muddathir

Translation of the Meanings of Surah Muddathir in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Muddathir translated into Swahili, Surah Al-Muddaththir in Swahili. We provide accurate translation of Surah Muddathir in Swahili - السواحيلية, Verses 56 - Surah Number 74 - Page 575.

بسم الله الرحمن الرحيم

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ (1)
Ewe uliye jigubika
قُمْ فَأَنذِرْ (2)
Simama uonye
وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ (3)
Na Mola wako Mlezi mtukuze
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ (4)
Na nguo zako, zisafishe
وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ (5)
Na yaliyo machafu yahame
وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ (6)
Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa
وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ (7)
Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri
فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ (8)
Basi litapo pulizwa barugumu
فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ (9)
Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu
عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ (10)
Kwa makafiri haitakuwa nyepesi
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا (11)
Niache peke yangu na niliye muumba
وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا (12)
Na nikamjaalia awe na mali mengi
وَبَنِينَ شُهُودًا (13)
Na wana wanao onekana
وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا (14)
Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ (15)
Kisha anatumai nimzidishie
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا (16)
Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu
سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا (17)
Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana
إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ (18)
Kwani hakika yeye alifikiri na akapima
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ (19)
Basi ameangamia! Vipi alivyo pima
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ (20)
Tena ameangamia! Vipi alivyo pima
ثُمَّ نَظَرَ (21)
Kisha akatazama
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ (22)
Kisha akakunja kipaji, na akanuna
ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ (23)
Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari
فَقَالَ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ (24)
Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa
إِنْ هَٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ (25)
Haya si chochote ila kauli ya binaadamu
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ (26)
Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ (27)
Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar
لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ (28)
Haubakishi wala hausazi
لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ (29)
Unababua ngozi iwe nyeusi
عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ (30)
Juu yake wapo kumi na tisa
وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ (31)
Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu
كَلَّا وَالْقَمَرِ (32)
Hasha! Naapa kwa mwezi
وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ (33)
Na kwa usiku unapo kucha
وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ (34)
Na kwa asubuhi inapo pambazuka
إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ (35)
Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa
نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ (36)
Ni onyo kwa binaadamu
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ (37)
Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa
كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ (38)
Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma
إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ (39)
Isipo kuwa watu wa kuliani
فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ (40)
Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
عَنِ الْمُجْرِمِينَ (41)
Khabari za wakosefu
مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ (42)
Ni nini kilicho kupelekeni Motoni
قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ (43)
Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali
وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ (44)
Wala hatukuwa tukiwalisha masikini
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ (45)
Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ (46)
Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo
حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ (47)
Mpaka yakini ilipo tufikia
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ (48)
Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi
فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ (49)
Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili
كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ (50)
Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa
فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ (51)
Wanao mkimbia simba
بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً (52)
Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa
كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ (53)
Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera
كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ (54)
Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ (55)
Basi anaye taka atakumbuka
وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ (56)
Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas