×

Surah An-Naba in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah An Naba

Translation of the Meanings of Surah An Naba in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah An Naba translated into Swahili, Surah An-Naba in Swahili. We provide accurate translation of Surah An Naba in Swahili - السواحيلية, Verses 40 - Surah Number 78 - Page 582.

بسم الله الرحمن الرحيم

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ (1)
WANAULIZANA nini
عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ (2)
Ile khabari kuu
الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ (3)
Ambayo kwayo wanakhitalifiana
كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (4)
La! Karibu watakuja jua
ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (5)
Tena la! Karibu watakuja jua
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا (6)
Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko
وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا (7)
Na milima kama vigingi
وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا (8)
Na tukakuumbeni kwa jozi
وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا (9)
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا (10)
Na tukaufanya usiku ni nguo
وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا (11)
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha
وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا (12)
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu
وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا (13)
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto
وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا (14)
Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni
لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا (15)
Ili tutoe kwayo nafaka na mimea
وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا (16)
Na mabustani yenye miti iliyo kamatana
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا (17)
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake
يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا (18)
Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi
وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا (19)
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا (20)
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا (21)
Hakika Jahannamu inangojea
لِّلطَّاغِينَ مَآبًا (22)
Kwa walio asi ndio makaazi yao
لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا (23)
Wakae humo karne baada ya karne
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا (24)
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji
إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا (25)
Ila maji yamoto sana na usaha
جَزَاءً وِفَاقًا (26)
Ndio jaza muwafaka
إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا (27)
Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu
وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا (28)
Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu
وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا (29)
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika
فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا (30)
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا (31)
Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu
حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا (32)
Mabustani na mizabibu
وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا (33)
Na wake walio lingana nao
وَكَأْسًا دِهَاقًا (34)
Na bilauri zilizo jaa
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا (35)
Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo
جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا (36)
Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha
رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا (37)
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake
يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا (38)
Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu
ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا (39)
Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi
إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا (40)
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas