Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 53 - يُونس - Page - Juz 11
﴿۞ وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ ﴾
[يُونس: 53]
﴿ويستنبئونك أحق هو قل إي وربي إنه لحق وما أنتم بمعجزين﴾ [يُونس: 53]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hao washirikina miongoni mwa watu wako, ewe Mtume, wanataka uwape habari kuhusu adhabu Siku ya Kiyama, «Je, ni kweli hiyo? Waambie, ewe Mtume, «Ndio, naapa kwa Mola wangu, hiyo ni kweli isiokuwa na shaka.Na nyinyi si wenye kumlemea Mwenyezi Mungu Asiwafufue na kuwalipa, kwani nyinyi muko kwenye udhibiti wa Mwenyezi Mungu na mamlaka Yake |