Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 71 - يُونس - Page - Juz 11
﴿۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ ﴾
[يُونس: 71]
﴿واتل عليهم نبأ نوح إذ قال لقومه ياقوم إن كان كبر عليكم﴾ [يُونس: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wasimulie, ewe Mtume, makafiri wa Maka habari ya Nūḥ, amani imshukiye, pamoja na watu wake alipowaambia, «Ikiwa imekuwa ni uzito kwenu kukaa kwangu na nyinyi kuwakumbusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, basi ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mategemeo yangu, na matumaini yangu yako Kwake Yeye. Basi tayarisheni mambo yenu na waiteni washirika wenu, kisha msiyafanye mambo yenu yafichike bali yawe waziwazi yenye kuonekana, kisha amueni juu yangu mateso na mabaya mnayoyaweza wala msinipe muhula wa saa moja ya mchana |