Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 73 - يُونس - Page - Juz 11
﴿فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ ﴾
[يُونس: 73]
﴿فكذبوه فنجيناه ومن معه في الفلك وجعلناهم خلائف وأغرقنا الذين كذبوا بآياتنا﴾ [يُونس: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi wakamkanusha Nūḥ, watu wake katika yale Aliyowaitia kwayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo tulimuokoa Yeye na waliokuwa na Yeye kwenye jahazi, na tukawafanya wao washikilie nafasi ya waliokanusha katika ardhi, na tukawazamisha wale waliokataa hoja zetu. Hivyo basi, fikiria, ewe Mtume, namna ulivyokuwa mwisho wa watu wale ambao Mtume wao Aliwaonya adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake |