Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 100 - هُود - Page - Juz 12
﴿ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ ﴾
[هُود: 100]
﴿ذلك من أنباء القرى نقصه عليك منها قائم وحصيد﴾ [هُود: 100]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haya tuliyokutajia wewe, ewe Mtume, ni miongoni mwa habari za watu wa miji ambayo tuliwaangamiza watu wake, twakupasha habari zake. Na miongoni mwa miji hiyo kuna iliyo na athari zilizosalia; na miongoni mwazo kuna ambazo athari zake zimefutika, hakuna chochote katika hizo kilichosalia |