Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 44 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَقِيلَ يَٰٓأَرۡضُ ٱبۡلَعِي مَآءَكِ وَيَٰسَمَآءُ أَقۡلِعِي وَغِيضَ ٱلۡمَآءُ وَقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَٱسۡتَوَتۡ عَلَى ٱلۡجُودِيِّۖ وَقِيلَ بُعۡدٗا لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[هُود: 44]
﴿وقيل ياأرض ابلعي ماءك وياسماء أقلعي وغيض الماء وقضي الأمر واستوت على﴾ [هُود: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akasema Mwenyezi Mungu kuiambia ardhi, baada ya watu wa Nūḥ kuangamia, «Ewe ardhi! Kunywa maji yako. Na ewe mbingu! Simamisha kunyesha mvua.» Na maji yakapungua na yakanywea, na amri ya Mwenyezi Mungu ikapitishwa ya kuangamia watu wa Nūḥ, na jahazi ikaegesha juu jabali la Jūdīy. Na hapo kukasemwa, «Kuwa mbali (na rehema ya Mwenyezi Mungu) ni kwa wale madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wasiamini.» |