Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 80 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿فَلَمَّا ٱسۡتَيۡـَٔسُواْ مِنۡهُ خَلَصُواْ نَجِيّٗاۖ قَالَ كَبِيرُهُمۡ أَلَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ أَبَاكُمۡ قَدۡ أَخَذَ عَلَيۡكُم مَّوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبۡلُ مَا فَرَّطتُمۡ فِي يُوسُفَۖ فَلَنۡ أَبۡرَحَ ٱلۡأَرۡضَ حَتَّىٰ يَأۡذَنَ لِيٓ أَبِيٓ أَوۡ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ لِيۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ ﴾
[يُوسُف: 80]
﴿فلما استيأسوا منه خلصوا نجيا قال كبيرهم ألم تعلموا أن أباكم قد﴾ [يُوسُف: 80]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walipokata tamaa ya kukubali kwake matakwa yao, walikaa kando na watu wakawa wanashauriana baina yao. Mkubwa wao kimyaka alisema, «Je hamjui kuwa baba yenu alichukuwa kwenu ahadi ya mkazo kuwa mtamrudisha ndugu yenu mpaka mshindwe, Na kabla ya tukio hili mlifanya kasoro kuhusu Yūsuf na mkamzungukia kinyume kwa hiana. Kwa hivyo sitaondoka kwenye ardhi ya Misri mpaka baba yangu aniamuru niondoke au Mola wangu Anihukumie niondoke na niweze kumchukua ndugu yangu. Na Mwenyezi Mungu ni Bora wa wanaohukumu na ni muadilifu zaidi wa wenye kutoa uamuzi baina ya watu |