Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 5 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿۞ وَإِن تَعۡجَبۡ فَعَجَبٞ قَوۡلُهُمۡ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍۗ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَاقِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ﴾
[الرَّعد: 5]
﴿وإن تعجب فعجب قولهم أئذا كنا ترابا أئنا لفي خلق جديد أولئك﴾ [الرَّعد: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ukiona ajabu , ewe Mtume, ya makafiri kutoamini baada ya dalili hizi, basi ajabu kubwa zaidi ni kusema kwao, «Je, tukifa na tukawa mchanga tutafufuliwa upya?» Hao ndio wenye kumkanusha Mola wao Aliyewafanya waweko kutoka kwenye hali ya kutokuwako. Na hao kutakuwa na minyororo kwenye shingo zao Siku ya Kiyama. Na hao wataingia Motoni na hawatatoka kabisa |