Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 1 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿الٓرۚ كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ لِتُخۡرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ ﴾
[إبراهِيم: 1]
﴿الر كتاب أنـزلناه إليك لتخرج الناس من الظلمات إلى النور بإذن ربهم﴾ [إبراهِيم: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Alif, Lām, Rā. Hii Qur’ani ni kitabu tulichokuletea wahyi ili uwatoe binadamu kutoka kwenye upotevu na upotovu kuwapeleka kwenye uongofu na mwangaza, kwa idhini ya Mola wao na taufiki Yake kwao, kwenye Uislamu ambao ndio njia ya Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda Anayehimidiwa kwa kila hali |