Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 2 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿ٱللَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ مِنۡ عَذَابٖ شَدِيدٍ ﴾
[إبراهِيم: 2]
﴿الله الذي له ما في السموات وما في الأرض وويل للكافرين من﴾ [إبراهِيم: 2]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Ambaye ni Vyake vilivyoko mbinguni na vya ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuviendesha. Yeye Ndiye Ambaye ni lazima ibada Afanyiwe Yeye Peke Yake. Na wale waliogeuka na wasimuamini Mwenyezi Mungu na wasiwafuate Mitume Wake watapata maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama |