Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 5 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ أَنۡ أَخۡرِجۡ قَوۡمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرۡهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ ﴾
[إبراهِيم: 5]
﴿ولقد أرسلنا موسى بآياتنا أن أخرج قومك من الظلمات إلى النور وذكرهم﴾ [إبراهِيم: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kwa hakika tulimtuma Mūsā kwa Wana wa Isrāīl na tukamsaidia kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake na tukammpa amri awalinganie wao kwenye Imani, ili awatoe wao kutoka kwenye upotevu awatie kwenye uongofu na awakumbushe neema za Mwenyezi Mungu na mateso Yake katika wakati wake. Katika kukumbusha huku mambo hayo kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, kuyaepuka yaliyoharamishwa na Yeye na kuyakubali maandiko Yake, mwenye kushukuru sana, mwenye kusimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na anayemshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema Zake. Aina mbili hizi za watu zimetajwa mahsusi, kwa kuwa wao ndio wanaozingatia hizo dalili na hawaghafiliki nazo |