Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 93 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[النَّحل: 93]
﴿ولو شاء الله لجعلكم أمة واحدة ولكن يضل من يشاء ويهدي من﴾ [النَّحل: 93]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau Mwenyezi Mungu angalitaka angaliwaafikia nyote Akawafanya muwe kwenye muelekeo mmoja, nao ni Uislamu na Imani, na Angaliwalazimisha nao. Lakini Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Anampoteza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa walichagua upotevu, Asimuongoze kwa uadilifu Wake. Na Anamuongoza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa wao walichagua haki, Akampa muelekeo kwa wema Wake. Na Mwenyezi Mungu Atawauliza nyinyi nyote, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkiyafanya ulimwenguni kati ya yale Aliyowaamrisha nayo na Aliyowakataza, na Atawalipa nyinyi kwa hayo |