Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 92 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِي نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثٗا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ ﴾
[النَّحل: 92]
﴿ولا تكونوا كالتي نقضت غزلها من بعد قوة أنكاثا تتخذون أيمانكم دخلا﴾ [النَّحل: 92]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msirudi nyuma kwenye ahadi zenu, ukawa mfano wenu ni kama wa mwanamke aliyefuma mfumo akautengeneza vizuri kisha akaufumua, Mnavifanya viapo vyenu mlivyoviapa wakati wa makubaliano kuwa ni udanganyifu kwa mliyopatana naye, mkawa mnazivunja ahadi zenu mnapopata kundi la watu wenye mali kuliko wale mlioahidiana nao. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu Anawapa mtihani kwa kuwaamrisha nyinyi mtekeleze ahadi na kuwakataza nyinyi msizivunje. Na ili Apate kuwaeleza, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkitafautiana kwayo kuhusu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuuamini unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |