Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 83 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَإِذَآ أَنۡعَمۡنَا عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ أَعۡرَضَ وَنَـَٔا بِجَانِبِهِۦ وَإِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ كَانَ يَـُٔوسٗا ﴾
[الإسرَاء: 83]
﴿وإذا أنعمنا على الإنسان أعرض ونأى بجانبه وإذا مسه الشر كان يئوسا﴾ [الإسرَاء: 83]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tunapompa mwanadamu, vile alivyo, neema ya mali na afya na mfano wa hizo, anageuka na kujiweka mbali na kumtii Mwenyezi Mungu, na akipatikana na shida ya ufukara au ugonjwa huwa ni mwenye kukata tamaa, kwa kuwa yeye haamini kuwa atapata nyongeza njema za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemuhifadhi katika hali yake ya raha na ya shida |