Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 109 - الكَهف - Page - Juz 16
﴿قُل لَّوۡ كَانَ ٱلۡبَحۡرُ مِدَادٗا لِّكَلِمَٰتِ رَبِّي لَنَفِدَ ٱلۡبَحۡرُ قَبۡلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَٰتُ رَبِّي وَلَوۡ جِئۡنَا بِمِثۡلِهِۦ مَدَدٗا ﴾
[الكَهف: 109]
﴿قل لو كان البحر مدادا لكلمات ربي لنفد البحر قبل أن تنفد﴾ [الكَهف: 109]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtuume, «Lau maji ya bahari yalikuwa wino wa kalamu za kuandikia maneno ya Mwenyezi Mungu yanayokusanya elimu Yake, hukumu Zake na yale Aliyowatumia wahyi Malaika Wake na Mitume Wake, yangaliisha maji ya bahari kabla maneno ya Mwenyezi Mungu hayajaisha, hata kama tulikuja na bahari nyingine za kuongezea mfano wa bahari hiyo. Katika aya hii pana kuthibitisha kikweli sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama kunakonasibiana na utkufu Wake na ukamilifu Wake.» |