Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 17 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿۞ وَتَرَى ٱلشَّمۡسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَٰوَرُ عَن كَهۡفِهِمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقۡرِضُهُمۡ ذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَهُمۡ فِي فَجۡوَةٖ مِّنۡهُۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِۗ مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ وَلِيّٗا مُّرۡشِدٗا ﴾
[الكَهف: 17]
﴿وترى الشمس إذا طلعت تزاور عن كهفهم ذات اليمين وإذا غربت تقرضهم﴾ [الكَهف: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Walipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu Aliwatia usingizi wakalala na Akawahifadhi. Na utaliona jua, ewe mwenye kuwatazama wao, linapochomoza upande wa mashariki linapenyeza pale walipo upande wa kulia, na linapozama linawaacha upande wa kushoto, na hali wao wako kwenye sehemu kunjufu ndani ya pango, joto la jua haliwasumbui na hewa haiwakatikii. Hayo tuliyowafanyia vijana hawa ni miongoni mwa dalili za uweza wa wa Mwenyezi Mungu. Basi yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Atamuafikia kuongoka kwa aya Zake, yeye ndiye mwenye kuongoka, na yoyote ambaye Hatamuafikia hilo, hutapata yoyote wa kumsaidia na kumuongoza kuifikia haki, kwani kuafikiwa na kutoafikiwa viko mikononi mwa Mwenyezi Mungu |