Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 18 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَتَحۡسَبُهُمۡ أَيۡقَاظٗا وَهُمۡ رُقُودٞۚ وَنُقَلِّبُهُمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَذَاتَ ٱلشِّمَالِۖ وَكَلۡبُهُم بَٰسِطٞ ذِرَاعَيۡهِ بِٱلۡوَصِيدِۚ لَوِ ٱطَّلَعۡتَ عَلَيۡهِمۡ لَوَلَّيۡتَ مِنۡهُمۡ فِرَارٗا وَلَمُلِئۡتَ مِنۡهُمۡ رُعۡبٗا ﴾
[الكَهف: 18]
﴿وتحسبهم أيقاظا وهم رقود ونقلبهم ذات اليمين وذات الشمال وكلبهم باسط ذراعيه﴾ [الكَهف: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na utadhani, ewe mwenye kutazama, kwamba watu wa pangoni wako katika hali ya kuangaza, na mambo yalivyo ni kuwa wao wamelala, na sisi tunawaangalia kwa kuwatunza, tunawageuza na wao wamelala, mara nyingine ubavu wa kulia na mara nyingine ubavu wa kushoto, ili ardhi isiwale, na mbwa wao aliyekuwa amefuatana nao ameinyosha miguu yake ya mbele kwenye ukumbi wa pango. Lau uliwashuhudia ungaligeuka kukimbia na unagalijawa na kicho kwa kuwaogopa |