Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 46 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿ٱلۡمَالُ وَٱلۡبَنُونَ زِينَةُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابٗا وَخَيۡرٌ أَمَلٗا ﴾
[الكَهف: 46]
﴿المال والبنون زينة الحياة الدنيا والباقيات الصالحات خير عند ربك ثوابا وخير﴾ [الكَهف: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mali na watoto ni uzuri na nguvu za ulimwengu huu wenye kumalizika. Na matendo mema, hasa kuleta tasbihi (kusema Subḥāna-llāh), tahmidi (kusema Alḥmdu li-llāh), takbiri (kusema Allāh Akbar) na tahlili(kusema Lā ilāha illa-llāh) yana malipo mazuri zaidi kuliko mali na wana. Matendo haya mema ndio bora zaidi kwa mtu kutarajia malipo mema kutoka kwa Mola wake na akapata kwayo huko Akhera yale ambayo alikuwa akiyatazamia duniani |