Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 45 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَآءٍ أَنزَلۡنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخۡتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلۡأَرۡضِ فَأَصۡبَحَ هَشِيمٗا تَذۡرُوهُ ٱلرِّيَٰحُۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقۡتَدِرًا ﴾
[الكَهف: 45]
﴿واضرب لهم مثل الحياة الدنيا كماء أنـزلناه من السماء فاختلط به نبات﴾ [الكَهف: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wapigie watu, ewe Mtume, hasa wale wenye kujiona kati yao, mfano wa hali ya ulimwengu, ambao wameghurika nao, kwa uzuri wake na upesi wa kuondoka kwake, kwamba ni kama maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka juu ambayo kwayo mimea ikatoka kwa idhini Yake na ardhi ikageuka ikawa rangi kijani. Na usipite isipokuwa muda mchache kitahamaka mimea hii ikawa imevunjikavunjika inarushwa na upepo kila upande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza mkubwa juu ya kila kitu |