Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 52 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿وَيَوۡمَ يَقُولُ نَادُواْ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُمۡ فَدَعَوۡهُمۡ فَلَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُمۡ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَهُم مَّوۡبِقٗا ﴾
[الكَهف: 52]
﴿ويوم يقول نادوا شركائي الذين زعمتم فدعوهم فلم يستجيبوا لهم وجعلنا بينهم﴾ [الكَهف: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wakumbushe pindi Atakaposema Mwenyezi Mungu kuwaambia washirikina Siku ya Kiyama, «Waiteni washirika wangu ambao mlikuwa mnadai kwamba wao ni washirika wangu katika ibada, wapate kuwaokoa na mimi leo.» Hapo wakaomba uokozi wao, na wao wasiwaokoe, na tukaweka baina ya wenye kuabudu na waabudiwa kitu cha kuwaangamiza katika moto wa Jahanamu wawe wote ni wenye kuangamia humo |