Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 110 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ﴾
[البَقَرَة: 110]
﴿وأقيموا الصلاة وآتوا الزكاة وما تقدموا لأنفسكم من خير تجدوه عند الله﴾ [البَقَرَة: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Jishughulisheni, enyi Waumini, kutekeleza Swala kwa namna sahihi ipasavyo na kutoa Zaka zilizofaradhiwa. Na mjue kwamaba kila kheri mnayoitangulizia nafsi zenu, mtapata thawabu zake Akhera mbele ya Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye Aliyetukuka ni Mwenye kuyaona matendo yenu na Atawalipa kwayo |